Article Rights Miaka Chini Ya 18, Onyesho 3


Script, Drama, Miaka Chini Ya 18, Onyesho 3












Ndani, chumba cha hospitali mchana. Tabu na mtoto wamepumzika kitandani. Pembeni Mama Visa anambusu mtoto na kumbusu Tabu.

"Hongera. Umepata mtoto wa kiume. Mtoto mkubwa!" Mama Visa anamrudishia mtoto kwa Tabu ambaye anampokea.
"Ndiyo sababu alikutesa sana. Utamwita nani?".
"Mimba hii imenitesa sana, mwishoni mambo yote yamekuwa salama. Namshukuru Mungu! Kwa hiyo ataitwa Mateso".
 Mama Visa anaonyesha wasi wasi. " Uwe mwangalifu na majina haya ambayo yanaleta bahati mbaya siku zote za baadaye!" anamwambia rafiki yake.
"Usijali" Tabu anamjibu.