Article Rights Miaka Chini Ya 18, Onyesho 1


Script, Drama, Miaka Chini Ya 18, Onyesho 1












Onyesho 1

Ni Usiku, nje, njiani kwenda hospital Usiku, Mama Visa na Tabu wanawahi hospitlini. Tabu ana mimba akiwa na uchungu amemwegemea Mama Visa.Kuna mawingu mazito angani, na uso wa Tabu unaonyesha kiasi cha uchungu alicho nacho.

"Jitahidi shoga yangu, tumekaribia kufika hospitali." Mama Visa anamwambia.

Tabu anakighughumia kwa machungu. "Nimechoka sana Mama Visa. Ningekuwa na uwezo ningejitua mzigo huu sasa hivi" anamjibu.
"Hatujafika bado. Jitahidi" Mama Visa anamjibu. Kuwa mwanamke ni ujasiri. Baada ya hapo hutasahau mateso yako yote tabu. Ndiyo, utasahau!
Tabu anainama kwa machungu, akiwa amechuchumaa. Macho ya Mama Visa yanaangalia mbinguni na mvua inaanza kunyesha. Wanaendelea kutembea hdi wafike mlango wa hospitali na kuingia.