Article Rights Miaka Chini Ya 18, Onyesho 5

Drama, Human Rights, Miaka Chini Ya 18, Onyesho 5


Miaka Chni Ya18, Scene 5, by Ucip Zabit

Nje, asubui, Tabu amekaa anachambua mchicha. Sura yake imeharibiwa vibaya. Mama Visa anafika na kustaajabu anapomuona rafiki yake. "Nimekuta hii chini ya mlango wangu leo" anatangaza, huku akionyesha kipande cha karatasi na kuanza kuisoma. “Nimemuua mke wangu, na mtoto wake pia. Msinitafute naondoka! Shemeji.Ina maana gani hii?" anauliza.

"Ni kama unavyoona." anamjibu Tabu. "Mahusiano mengine yalioshindikana".
Mateso anatoka nje. Anamajiraha usoni ya kipigo cha mpenzi wake Mama yake, na amebeba begi. "Mama
naondoka." anatangaza na yeye.
Tabu anamwangalia kwa upole. "Unaenda wapi mtoto wangu?" anamuliza.
"Sina uhakika, lakini sitarudi mpaka nitakapokua mtu mzima na kupata hela za kututosha mimi na wewe."
Mateso anamjibu kwa uhakika.
Tabu anasimama. "Hapana mateso, bado uko shule, bado ni mwanafunzi."
"Hapana Mama. Siwezi kukuona ukiteseka bila kufanya jambo lolote. Naondoka. Nakupenda." Mateso anamjibu. Anaondoka.
"Unaenda wapi namna hiyo?" Tabu anabembeleza. "Nakuomba usiondoke. Mateso rudi sasa hivi. Bado ni mtoto mdogo. Wewe ni mtoto wangu." anafoka. "Mama Visa, nisaidie!"
Mateso anaondoka taratibu. Tabu anamuangalia na kuanza kulia.Mama Visa anatingisha kichwa.